Posts
Showing posts from July, 2019
REHEMA WA NJIA PANDA SEHEMU YA TANO
- Get link
- X
- Other Apps
''Asante Mungu ameamka! Kisebengo na mwenzake walijikuta wakiongea kwa sauti ya juu iliyowashtua hata wagonjwa wenzake. ''Kweli Mungu mkubwa hakuwa wakupona yule''Alisikika mgonjwa alikuwa kwenye kitanda cha tatu kutoka alipokuwa amelazwa Anord. ''Maombi yamesaidia unafikiri bila kuomba angepona kweli?" Alisikika mwingine. ''Hebu nielezeni ilikuwaje?"Anord aliongea kwa kunong'oneza akimuuliza Kisebengo wakati huo akiwa amesahau kabisa ugomvi wao wa asubuhi. ''Nitakuambia ukiruhusiwa ila kiukweli haupo sawa yaani unaonekana una jini linakutesa bora tuu utembee?" Yule mfanyakazi mwingine aliongea akimkumbusha maneno ya Kisebengo ya asubuhi lakini tofuti na wakati ule Anord alionekakana kuyatafakari maneno ambayo haikuwa mara yake ya kwanza ama ya pili kuyasikia. ''Kutembea?" ''Ndiyo'' ''Mhhh kwani tatizo nini?"Anord alikumbuka raha ambazo alipanga akampe Siku
REHEMA WA NJIA PANDA SEHEMU YA 4
- Get link
- X
- Other Apps
Siku iliyofuata ndugu na jamaa kutoka sehemu mbalimbali walikuja kujumuika na wafanyakazi wengine kuuweka mwili ule kwenye nyumba yake ya milele. Hakuna aliyejua kilichokuwa nyuma ya ile ajali wengi wakiamini ilikuwa ni ajali ya kawaida iliyokuwa imetokana na mwendokasi. Siku, wiki na hatimaye miezi ilipita lakini kidonda kilichotokana na jeraha la ajali kiliendelea kuongezeka na kutoa harufu kali iliyopekelea watu kuogopa kuwa karibu ya Anord.Japokuwa mwenyewe alidai kuwa alikuwa hapati maumivu yoyote lakini wenzake walidai kichwa chake kilikuwa hatarini sana kutokana na hali yake. Wakati hayo yakiendelea ile ndoto tamu ilikuwa ikijirudia kila siku lakini hakuna siku aliyokuwa amefanikiwa kufikia hatua ya kulila tunda.Ndoto haikuchagua sehemu ya kutokea nyumbani ndani ya gari ofisini na popote pale ilipojisikia kutokea. Kila mara Anord alijikuta akiaibika kuchafua nguo zake kwa madafu lakini licha ya aibu ile aliifurahia ile ndoto na kutamani imtokee tena. Saut