REHEMA WA NJIA PANDA SEHEMU YA 4


Siku iliyofuata ndugu na jamaa kutoka sehemu mbalimbali walikuja kujumuika na wafanyakazi
wengine kuuweka mwili ule kwenye nyumba yake ya milele.
Hakuna aliyejua kilichokuwa nyuma ya ile ajali wengi wakiamini ilikuwa ni ajali ya kawaida
iliyokuwa imetokana na mwendokasi.
Siku, wiki na hatimaye miezi ilipita lakini kidonda kilichotokana na jeraha la ajali kiliendelea
kuongezeka na kutoa harufu kali iliyopekelea watu kuogopa kuwa karibu ya Anord.Japokuwa
mwenyewe alidai kuwa alikuwa hapati maumivu yoyote lakini wenzake walidai kichwa chake
kilikuwa hatarini sana kutokana na hali yake.
Wakati hayo yakiendelea ile ndoto tamu ilikuwa ikijirudia kila siku lakini hakuna siku aliyokuwa
amefanikiwa kufikia hatua ya kulila tunda.Ndoto haikuchagua sehemu ya kutokea nyumbani
ndani ya gari ofisini na popote pale ilipojisikia kutokea.
Kila mara Anord alijikuta akiaibika kuchafua nguo zake kwa madafu lakini licha ya aibu ile
aliifurahia ile ndoto na kutamani imtokee tena.
Sauti za kugugumia utamu ndizo zilizokuwa sababu ya wafanyakazi waliokuwa ama juu yake au
chini yake kupata cha kuongea ili atoke.
" Hivi unajua Anord amekuwa kichaa?" Katibu wa Anord alikuwa aakimweleza mfanyakazi
mwenzake.
''Yule atakuwa na jini asipotembea atapata shida au kufa kifo kibaya....''Alimjibu mwenzake
ambaye kabla ya kumalizia jibu lake alimwona Anord ambaye alionekana amesikia kila kitu.
''Umesema nini?"Anord aliuliza akiwa amefura kwa hasira.
''Sijasema kitu mbona umefura hivi?"Alijibiwa Anord jibu ambalo halikumwingia kabisa akilini.
" Nitapiga mtu hapa si mmesema habari za wehu na majini yenu?"
"Utakuwa umesikia vibaya hatujasema habari hizo ndugu''
"Halafu we mfupi ka Kisebengo unajifanya unajua kiherehere sana'' Anord alionekana kutokuwa
na mchezo hata kidogo akimsogelea mfanyakazi mwenzake aliyekuwa akipendelea kumwita
Kisebengo kutoka na kimo chake kifupi.
''Jamani mbona unapenda sana kunionea jamani ''Kisebengo alimlalamikia Anord ambaye
walitofautiana tuu vitengo ye akiwa mhasibu wa mkoa.
Japokuwa wote walionekana ni vijana wa rika moja Anord daima alionekana mwenye mamlaka
juu ya wenzake kwanza kutokana na kuwa na muda mrefu kwenye ile ofisi huku yeye akifanya
kazi zote kama mhasibu na afisa manunuzi wa mkoa wa Tabora.
''Samahani jamani lakini jiangalie Anord haya mambo si ya kawaida''Yule mfanyakazi mwingine
alishauri akimtetea Kisebengo na kumpa ukweli Anord ambaye kila mtu pale ofisini alijua kuwa
alikuwa kwenye matatizo makubwa.
''Na we unanitafuta kila siku ''
''Nani mimi"
''Ndiyo kila siku kazi kuwateta wenzako tuu na kuingilia hata yasokuhusu''
''Eti jamani mie kosa langu nini ?"
''Hulijui kosa lako ehhe ?"
''Ndiyo, au nilivyokushauri?''
''Umenishauri zaidi ya kuongea mambo ya kuongea wanawake?"Anord alionekana kupandwa na
jazba kabisa yaani hata mtu angemwita jina lake kwa wakati ule lazima angemgeuzia kibao na
kumchapa.
''He! Na wewe ukiwa na shida tusikuambie? Ngoja tuu tukuambie ukweli wewe una matatizo
makubwa kama ndugu na majirani zako wanaogopa kukuambia ukweli wakisubiri mahoka wa
babu zako wakuambie wanakupoteza nakuambia kwa mema kama utanichukia sawa ila hapa
umeshapata hasara''Kisebengo alijitutumua na kumwambia Anord ukweli ambao hakupenda
kabisa kuusikia kwani alihisi kuonewa.Kila neno lililokuwa likitafsiriwa na akili yake lilionekana kumchoma lakini si kwa kumfanya
awe mpole kwa kuwa ni la kweli bali lilikuwa likimpandisha hasira zake alijitahidi kujizuia
lakini hatimaye alijikuta akirusha konde lililokwepwa kiustadi na kisebengo ambaye aliliona
tangu likiandaliwa.
Anord hakukubali akatupa jiingine ambalo liliyompata Kisebengo kisawasawa kwani alionekana
kuzubaa baada ya kukwepa konde la kwanza.
Kisebengo alipelekwa mlangoni alikojipigiza na kupata maumivu ambayo yalimpandisha hasira.
Aliinuka na kumparamia Anord ambaye hakujiandaa kwa kumchapa ngumi ya uso iliyompata
sawasawa na kumpigiza ukutani na kutua chini kama mzigo jambo lililowafanya kisebengo na
mwenzake wapate hofu na kumwinua Anord ambaye alikuwa ameshapoteza fahamu.
Pona yao walikuwa watu watatu pekee kwani wafanyakazi wengine hawakuwepo mahali pale
ofisini kwa kuwa ilikuwa asubuhi sana tena Siku ya jumamosi ambayo haikuwa siku ya kazi kwa
ofisi nyingi pale mkoani na hata ofisi zilizokuwa zikitoa huduma zilichelewa kufunguliwa.
Akiwa katika kupoteza fahamu Sikujua alimtokea kama ndoto zake za siku zote lakini siku ile
alionekana mwenye furaha sana.
''Mbona unaonekana umefurahi sana mpenzi?" Anord aliuliza akimwangalia Sikujua kwa macho
ya uchu kwani alionekana amependeza kuliko Siku nyingine alizokuwa akimwota.
''Ninakucheka wewe''
''Mimi! Nachekesha?"
“Ndiyo unahangaika kufuta damu na kitambaaa ukihisi jasho"
''Kweli nilijua jasho kweli''Anord aligundua hilo baada ya kujiangalia mkono wake uliokuwa
unelowa damu, ajabu hakusikia maumivu yoyoyote.
''Hivi nimeumia sana?"
'Ndiyo lile kovu lako la ajali limefumuka tena, lakini tuachane na hayo leo ni siku ya furaha sana
maana ni siku ambayo nitakuwa na wewe wakati wote maishani mwangu''
''Kweli ?"Anord aliuliza kwa wahka.
''Kweli mpenzi wangu utaishi nami milele na utaijua sababu ya haya yote.
Anord alifurahi sana kwani alijua raha alizokuwa akiziota muda mfupi na kukatishiwa utamu
njiani akuwa akizipata kila wakati.
''Au ni ule wakati ambao ulisema nitapata nafasi ya kufaidi tunda lako?".Anord aliuliza
akikumbuka kuwa aliambiwa muda ukifika hawataishia njiani wala kufaidi raha usingizini bali
wataishi duniani kama watu wengine wakifurahia raha lakini kwa sharti moja la Sikujua
kutoonekana nje na angewambia ukweli juu ya maisha yake.
''Bado muda kufika ila ni hatua kuelekea huko''.
Licha ya kuambiwa kuwa muda ulikuwa haujafika Anord aliona ni hatua nzuri kwani hakuna
kitu alichokifurahia kama kuja kupata uhuru wa kula tunda la Sikujua wa ndotoni.Alimsogelea
Sikujua na kumkumbatia na kwa kuwa alikuwa amemfundishwa mambo mengi Anord alijikuta
amebobea katika kumpeleka Sikujua panapohusika bila hata kutumia fimbo yake ya kurekebishia
tabia.
Alimmvua gauni lake refu lililokuwa nguo pekee iliyokuwa imeufunika mwili wake na kumbeba
na kumshusha kitandani kisha kumshika kiuno chake kuelekea bafuni jambo ambalo lilimshtua
sana Sikujua jambo ambalo Anord hakuligundua kwani akili yake ilikuwa katika kwenda
kuanzisha raha.
''Nisubiri nakuja mpenzi''Anord aliongea akirudi chumbani kupitia sebuleni jambo ambalo bila
kujua lilimtisha Sikujua na ambaye kwa hasira aliinuka na kumfuata Anord na kumpiga
mgongoni na kumshitua Anord aliyeshtukia yupo hospitalini huku mbele yake kukiwa na
Kisebengo na yule mfanyakazi mwenzake waliyekuwa wote kwenye ugomvi.

Comments

Popular posts from this blog