Posts
Showing posts from August, 2019
BAADA YA SALLAM KUTHIBITISHA KUONDOKA KWA HARMONIZE,WCB SASA ITAKUA NI MWENDO WA TUZO NA SHOW
- Get link
- X
- Other Apps
Ikiwa ni siku chache zimepita tangu Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam atangaze kuwa Harmonize yupo mbioni kutemana na lebo ya muziki ya WCB, Kiongozi huyo ametangaza habari njema kwa mashabiki wa WCB. Sallam Sharaff Sallam amesema kuwa kuanzia sasa ni mwendo wa kuchukua tuzo na shows za kutosha kutoka kwa wasanii waliochini ya Lebo hiyo. Kuwahakikishia hilo mashabiki wa WCB, Sallam amesema wiki hii Diamond Platnumz anaachia ngoma mpya. “Tumerudi kibiashara zaidi. Ni mwendo wa tuzo, Muziki na shows za kutosha. Diamond Platnumz anadondosha ngoma mpya wiki hii,“ameahidi Sallam kupitia ukurasa wake wa Instagram.
HARMONIZE AJITOA WCB
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya tetesi nyingi kusambaa mitandaoni kuwa msanii wa muziki Tanzania, Harmonize anataka kujitoa kwenye lebo ya muziki ya WCB, Hatimae ukweli umewekwa hadharani. Kwa mujibu wa Meneja wa Diamond Platnumz, Na moja ya viongozi wa WCB, Meneja Sallam amesema kuwa Harmonize ametuma maombi ya kuvunja mkataba na WCB. Sallam akiongelea zaidi sakata hilo, Amesema kuwa moyo wa Harmonize kwa sasa haupo kabisa WCB bali ni mkataba tu ndio unamuweka WCB. “Harmonize kwasasa hivi ndani ya moyo wake hayupo WCB, Kwanini nasema hivyo? Harmonize tayari ameshatuma maombi ya ku-terminate mkataba wake na WCB, Yupo tu kusubiri kupitia vifungu vyote vya mkataba ili kuvunja mkataba” amesema Sallam kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha Wasafi FM. Kwa upande mwingine, Sallam amempongeza Harmonize kwa njia ya busara aliyoitumia katika nia yake ya kutaka kujitoa WCB. Amesema yeye anaamini WCB imemkuza, Na amemtakia kila la kheri huko aendako pindi mkataba huo utakapovunjwa rasmi