BAADA YA SALLAM KUTHIBITISHA KUONDOKA KWA HARMONIZE,WCB SASA ITAKUA NI MWENDO WA TUZO NA SHOW

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam atangaze kuwa Harmonize yupo mbioni kutemana na lebo ya muziki ya WCB, Kiongozi huyo ametangaza habari njema kwa mashabiki wa WCB.
Sallam Sharaff
Sallam amesema kuwa kuanzia sasa ni mwendo wa kuchukua tuzo na shows za kutosha kutoka kwa wasanii waliochini ya Lebo hiyo.
Kuwahakikishia hilo mashabiki wa WCB, Sallam amesema wiki hii Diamond Platnumz anaachia ngoma mpya.
“Tumerudi kibiashara zaidi. Ni mwendo wa tuzo, Muziki na shows za kutosha. Diamond Platnumz anadondosha ngoma mpya wiki hii,“ameahidi Sallam kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Comments

Popular posts from this blog