HARMONIZE AJITOA WCB
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya tetesi nyingi kusambaa mitandaoni kuwa msanii wa muziki Tanzania, Harmonize anataka kujitoa kwenye lebo ya muziki ya WCB, Hatimae ukweli umewekwa hadharani.
Kwa mujibu wa Meneja wa Diamond Platnumz, Na moja ya viongozi wa WCB, Meneja Sallam amesema kuwa Harmonize ametuma maombi ya kuvunja mkataba na WCB.
Sallam akiongelea zaidi sakata hilo, Amesema kuwa moyo wa Harmonize kwa sasa haupo kabisa WCB bali ni mkataba tu ndio unamuweka WCB.
“Harmonize kwasasa hivi ndani ya moyo wake hayupo WCB, Kwanini nasema hivyo? Harmonize tayari ameshatuma maombi ya ku-terminate mkataba wake na WCB, Yupo tu kusubiri kupitia vifungu vyote vya mkataba ili kuvunja mkataba” amesema Sallam kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha Wasafi FM.
Kwa upande mwingine, Sallam amempongeza Harmonize kwa njia ya busara aliyoitumia katika nia yake ya kutaka kujitoa WCB.
Amesema yeye anaamini WCB imemkuza, Na amemtakia kila la kheri huko aendako pindi mkataba huo utakapovunjwa rasmi
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment