Posts
Showing posts from June, 2019
REHEMA WA NJIA PANDA(03)
- Get link
- X
- Other Apps
Miaka mitano baada ya kuanza kazi Anord alipatwa na ugonjwa wa ajabu.Ilikuwa Siku ya jumamosi kama kawaida yake alikuwa na mazoea ya kufanya ziara za kushitukiza kwenye ofisi zilizokuwa chini ya idara yake wilayani.Akiwa ndani ya gari la serikali ambalo lilitumika tangu zama za ukoloni Anord alimwona mtu ambaye kama aliwahi kumwona mahali. Akamwambia dereva wake asimamishe gari, kisha alishuka na kuelekea upande aliomwona yule mwanamke.Baada ya hatua kama tatu macho yake yakakutana na mwanamke aliyekuwa akimfuata akiwa amekaa chini ya mti wa maembe. Alijikuta akishindwa kabisa kusogea, akajaribu kunyanyua mdomo wake aseme kitu lakini mdomo wake nao ukawa mzito kutamka kitu .Wakabaki wakitazamana tuu bila kuongea chochote. Macho yao yalijaribu kuzungumza lakini nayo yalipoteza uwezo huo, kila alipojaribu kumwongelesha kwa macho alishindwa. Baada ya kuduwaa kwa takribani dakika mbili, hatimaye macho yao ama tuseme nafsi zao zikazungumza. “Njoo, mwenzako nateseka
REHEMA WA NJIA PANDA(02)
- Get link
- X
- Other Apps
Tumaini Martin wengi wakipenda kumwita Tuma alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto watano wa mzee Martin Kasuku na Lydia Kilongo waliokuwa wafanyabiashara mkoani Dodoma.Mzee Kilongo alikuwa miongoni mwa askari wastafu wa Jeshi la Wananchi aliyekuwa na cheo kikubwa jeshini. Alikuwa na watoto watoto wakiume wanne waliokuwa na sura za kutisha na mtoto mmoja wa kike ambaye alikuwa na sura nzuri illiyokuwa ikimvutia kila aliyeiona ama kusikia sifa zake.Wengi walimtuhumu Bi Lydia kuwa huenda alichepuka alivyoenda kuwasalimia wazazi wake huko Kyela kwani binti alikuwa mrembo haswa.Uzuri wake ulivumbuliwa tangu akiwa mdogo na kadri alivyokuwa akikua ndivyo vitu vingi vilivyokuwa vimejificha kwenye mwili wake vilijitokeza na kumfanya kila mzuri mjini pale alinganishwe kwanza na binti huyo ambaye aliiibua matumaini ya wazazi wake kupata mtoto wa kike na kupewa jina la Tumaini. Akiwa darasa la saba Tumaini alikuwa ni miongoni mwa wanawake waliokuwa wakifuatiliwa kimapenzi n
REHEMA WA NJIA PANDA(01)
- Get link
- X
- Other Apps
"Oyaa, madenti subirini abiria waingie.’’ ‘’We dogo nitakufumua hembu sogeza kongoro zako pembeni"zilikuwa ni miongoni mwa kauli zikaharishazo za makondakta kila asubuhi na mchana wanafunzi waelekeapo na watokapo shuleni.Ni wakati ambao makondakta wanakuwa na kiburi kwani wanakuwa na uhakika wa kuwapata abiria ambao wakati huo huwa wanaenda na kutoka kwenye mihangaiko ya kutafuta riziki. Matusi na kusukumwa na hata kichaniwa sare za shule ni mambo yaliyoonekana kuzoeleka masikioni na machoni mwa watu ingawa palikuwa na wachache waliokuwa wakikereka na hali hiyo huku kauli za kejeli kutoka kwa watu wengine zikiwakatisha tamaa watu hao walikuwa wakijaribu kuwatetea wanafunzi ambao serikali iliwapa haki ya kulipa nusu ya nauli ya kawaida. Hayo yote yalikuwa yakitokea katika kituo kidogo cha mabasi cha Njia ya Ng'ombe kilichokuwa nje kidogo ya mji wa Moshi. Miongoni mwa wahanga wa kauli na manyanyaso hayo alikuwa Rehema Martin aliyekuwa akisoma darasa la tano k