REHEMA WA NJIA PANDA(01)
- Get link
- X
- Other Apps
"Oyaa, madenti subirini abiria waingie.’’
‘’We dogo nitakufumua hembu sogeza kongoro zako pembeni"zilikuwa ni miongoni mwa kauli
zikaharishazo za makondakta kila asubuhi na mchana wanafunzi waelekeapo na watokapo
shuleni.Ni wakati ambao makondakta wanakuwa na kiburi kwani wanakuwa na uhakika wa
kuwapata abiria ambao wakati huo huwa wanaenda na kutoka kwenye mihangaiko ya kutafuta
riziki.
Matusi na kusukumwa na hata kichaniwa sare za shule ni mambo yaliyoonekana kuzoeleka
masikioni na machoni mwa watu ingawa palikuwa na wachache waliokuwa wakikereka na hali
hiyo huku kauli za kejeli kutoka kwa watu wengine zikiwakatisha tamaa watu hao walikuwa
wakijaribu kuwatetea wanafunzi ambao serikali iliwapa haki ya kulipa nusu ya nauli ya kawaida.
Hayo yote yalikuwa yakitokea katika kituo kidogo cha mabasi cha Njia ya Ng'ombe
kilichokuwa nje kidogo ya mji wa Moshi.
Miongoni mwa wahanga wa kauli na manyanyaso hayo alikuwa Rehema Martin aliyekuwa
akisoma darasa la tano katika shule ya msingi Kiwanja cha ndege karibu kabisa na kituo hicho
kidogo cha magari.Ni kama vile alikuwa na damu ya kunguni kwani alionekana kuchukiwa na
karibu kila konda aliyekuwa pale stendi.Hiyo yote ilitokana na tukio lake la kudai kuwa alikuwa
ameibiwa nauli ndani ya gari kila alipotakiwa kutoa nauli mara tano mfululizo tena kwenye
magari tofauti kitu kilichomfanya kila kondakta na hata madereva kutomruhusu kupanda garini
hata kama angewaonesha nauli kitendo chake cha kusafiri bure wiki nzima kilionekana
kuwachukiza hata wanafunzi wenzake ambao wakifika stendi ilikuwa ni lazima kwao
kumtambulisha kwa konda kuwa huyo ndo Rehema wa Njia panda kwani wiki alilokuwa
akisafiri bure kama mchezo kila walipofika eneo lililoitwa njia panda alipotakiwa kutoa nauli
alidai kuwa alikuwa ameibiwa hatimaye Rehema likawa jina lake na Njia panda likawa jina la
baba yake.
Baadaye ilikuwa ni vigumu kwake kupata gari la kupanda si asubuhi si mchana hata kama
angekuwa na nauli na kupelekea kufikia uamuzi wa kuanza kutembea kwa miguu mara chache
alibahatika kupata rifti mwenye magari mengine yasiyo ya abiria.
Kutoka kwao Rehema hadi shuleni alitumia saa moja na dakika kumi na tatu kutembea hivyo
alikuwa akifika shuleni na nyumbani kwa kuchelewa tena akiwa hoi hali iliyopekea kuanza
kushuka kitaaluma.
Alishawaeleza walimu wake na mama yake ambao walilipokea jambo hilo kwa namna tofauti,
kwa upande wa walimu hawakulipokea kwa umakini jambo hilo, kwanza kwa kuwa Rehema
hakuwa miongoni mwa watoto watu waliokuwa wakifahamika pale shuleni ama kwa mali za
wazazi wao au umaarufu wao pia hakuwa miongoni mwa wanafunzi walikuwa na akili sana
darasani hivyo mateso yalionekana ni haki yake kuipata.Kwa upande wa mama yake hakuwa na
cha kufanya ingawa ilimuumiza sana zaidi ya kumwombea kwa Mungu wake ambaye kwake
aliamini kama akimwadhibu kwa dhambi alizokuwa amezitenda ujanani ama aseme utotoni.
Alikumbuka historia yake iliyokuwa ikimuumiza siku zote huku akimwomba Mungu
kumuadhibu kwa namna yoyote lakini si kwa kumfanya mwanaye apitie maisha kama yake
akiwa hai ama akiwa mfu.Alijua kabisa hakumjua baba halisi wa mwanaye kutokana na
matumizi ya ujana wake.
Siku zilikatika huku Rehema akizidi kuporomoka kitaaluma kutokana na mateso aliyoyapata
kutembea masaa mawili na nusu kila siku ilikuwa ni zaidi ya mazoezi ya marathoni waliyokuwawakiyafanya wanariadha kila ilipokaribia machi kila mwaka.Marafiki wachache walianza kumpa
sapoti hasa nyakati za jioni ili kumpa faraja binti huyo ambaye hadi umri huo hakumfahamu kwa
jina wala sura baba yake ambaye mama yake alimwambia kuwa alifariki kwa ajali mbaya ya gari
iliyotokea siku mbili baada ya kuzaliwa kwake.
Alionekana ni mtu aliyekuwa na mateso makubwa sana kwa kila aliyemwangalia licha ya
kulazimisha tabasamu usoni pake ,tabasamu ambalo lilikosa afya liliupoteza uzuri wa sura yake
huku nywele zake ndefu nyeusi na rangi nyeupe iliyouficha weusi ulioonekana kwa mbali
kwenye ngozi yake vilimfanya kila mtu amuweke kwenye kundi la watu waliochanganya damu
ya kiafrika na kizungu.Lakini licha ya uchotara wake Rehema alionekana kuing'ang'ania sura ya
kirembo aliyokuwa nayo mama yake Tumaini Martin ambaye kama si moshi wa kuni wakati wa
kupika pombe ya kienyeji maarufu kwa jina la 'Dadii' ili kuikimu familia yake basi angekuwa
miongoni mwa kumi bora ya akina mama warembo mjini Moshi.Miaka thelathini na sita
aliyokuwa nayo aliiamini yeye pekee lakini kila aliyemwangalia alimwona kama binti wa miaka
kumi na tisa ama ishirini na mbili.
Hakuwa na mtoto ama ndugu mwingine pale Moshi zaidi ya bintiye Rehema ambaye tangu
akiwa mdogo alianza kukutana na mateso makali baada ya kuugua ugonjwa wa ajabu uliomfanya
avimbe kichwa upande mmoja. ...itaen(elea kesho

Comments
Post a Comment