REHEMA WA NJIA PANDA(02)


Tumaini Martin wengi wakipenda kumwita Tuma alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto watano
wa mzee Martin Kasuku na Lydia Kilongo waliokuwa wafanyabiashara mkoani Dodoma.Mzee
Kilongo alikuwa miongoni mwa askari wastafu wa Jeshi la Wananchi aliyekuwa na cheo
kikubwa jeshini.
Alikuwa na watoto watoto wakiume wanne waliokuwa na sura za kutisha na mtoto mmoja wa
kike ambaye alikuwa na sura nzuri illiyokuwa ikimvutia kila aliyeiona ama kusikia sifa
zake.Wengi walimtuhumu Bi Lydia kuwa huenda alichepuka alivyoenda kuwasalimia wazazi
wake huko Kyela kwani binti alikuwa mrembo haswa.Uzuri wake ulivumbuliwa tangu akiwa
mdogo na kadri alivyokuwa akikua ndivyo vitu vingi vilivyokuwa vimejificha kwenye mwili
wake vilijitokeza na kumfanya kila mzuri mjini pale alinganishwe kwanza na binti huyo ambaye
aliiibua matumaini ya wazazi wake kupata mtoto wa kike na kupewa jina la Tumaini.
Akiwa darasa la saba Tumaini alikuwa ni miongoni mwa wanawake waliokuwa wakifuatiliwa
kimapenzi na wanaume wengi mjini Dodoma.Wazee,vijana,matajiri ,masikini waliokuwa na kazi
na wale wenzangu na mimi akina pangu pakavu tia mchuzi walijaribu bahati yao suala
alilolifikisha kwa baba yake kupitia mama yake ambaye hakuacha kuwaadhibu vijana aliokuwa
akiwakuta na binti yake.
Siku moja jioni kama ilivyokuwa kawaida yake wakiwa jikoni na mama yake Tumaini
alionekana mtu mwenye wasiwasi sana hali iliyomfanya mama yake ahisi kuwa binti yake
alikuwa na jambo lililomfanya awe katika hali hiyo
Mbona hivyo Tuma, kuna tatizo?" Aliuliza Lydia.
“Hakuna tatizo mama “alijibu Tuma huku akizuia machozi kushuka.
"Niambie mwanangu mie ni mama yako niambie jambo likusumbualo
nitakusaidie"Alibembeleza mama yake.
“Hutoniamini mama"
"Niambie mwanangu nitakuamini, mangapi umeniambia nikakuamini?"
"Yote yalikuwa madogo hili hamtaliamini mama"
“Au ndo hao wanaume wa kila siku? We u mrembo lazima wakusumbue cha msingi
kuyazingatia tuliyokueleza umri na wakati haujafika mwanangu" mama mtu alizidi kutoa nasaha.
“Ndiyo wanaume mama"
"Wamekutisha"
"Hata hawanitishi, ila huyu wa leo amenitisha"
"Unamfahamu?"
"Ndiyo"
"Nani"
"Baba Zita"
"Acha kuchuma dhambi binti yangu, baba Zita mchungaji? We mtoto unataka kugombanisha
watu si bure"
"Ndo maaana nilise,,,,,,,"
"Kimya shetani wewe umetufanya watoto" Aliongea Bi Lydia kwa hasira akimalizia na kofi
lililokwepwa kiustadi na kutua juu ya sufuria iliyotoa ukelee baada ya kufika sakafuni na
kumshtua Mzee Martin aliyekuwa sebuleni na wanawe wa wawili mwisho na kuelekea jikoni.
Anord Mwakibale au Baba Zita kama wengi walivyozoea kumwita alikuwa Mchungaji wa
kanisa la "The End" lililokuwa limeingia nchini miaka ya tisini huku likisifika kwa kuwa
miongoni mwa makanisa machache yaliyokuwa na uwezo wa kuwaponya wagonjwa, kuwafanya vipofu waone, viziwi wakasikia na hata viwete wakatembea.
Mchungaji Mwakibale alifahamika si tuu Dodoma pekee bali hata nje ya Afrika kutokana na kazi yake kubwa ya kuokoa maelfu ya wanadamu waliokuwa na shida mbalimbali kwa miujiza na wokovu. Urafiki wake na Mzee Martin ulianza miaka mingi iliyopita kipindi wapo shule ya sekondari ya
wavulana Tabora.Walitengana kwenye mafunzo ya Jeshi La kujenga Taifa ambapo Martin
alipelekwa Oljoro na Anord akipelekwa Kanembwa.Walikuja tena kukutana chuo kikuu cha Dar
es salaam ambako waliurejesha urafiki wao hadi walipomaliza na Martin aliporejea jeshini kwa
Mara ya pili safari hii akiingia Jeshi la wananchi na Anord akipangiwa kazi mkoani Tabora kama Afisa manunuzi wa Mkoa.
Itaendelea

Comments

Popular posts from this blog