"ALCATRAZ" GEREZA HATARI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA ULIMWENGUNI.


@BY BIN CYPHER
Alcatraz lilikuwa gereza hatari na maarufu zaidi Nchini Marekani. Hapa ndipo nyumbani kwa watukutu walioshindikana wa Marekani miaka hiyo.
Alcatraz inapatikana katika jimbo la California kwenye kisiwa cha Alcatraz. Lilifunguliwa rasmi mwaka 1934 hadi mwaka 1935 tayari lilikuwa na wafungwa 242. Gereza hili lilifungwa rasmi tarehe 21 March 1963 hivyo lilidumu kwa miaka 29 tu.
Mambo yaliolifanya gereza hili kuwa maarufu zaidi ulimwenguni ni yafuatayo:
(A). Aina ya watuhumiwa waliopatikana humu
(B). Lilikuwa likizungukwa na bahari, pia ulinzi usiokifani.
(C). Mazingira na maisha ndani ya gereza lenyewe yalikuwa tatanishi yenye kuhitaji roho ngumu kuyavumilia.
HAWA NI BAADHI YA WATEMI WALIOWAHI KUFUNGWA GEREZA HILI.
I). George Kelly.
Huyu mtemi alifahamika kwa jina "The Machine Gun" alipewa jina hili kutokana na utundu wake kwenye zana hii wakati wa utekelezaji uhalifu wake. Huyu alikuwa kiongozi wa kundi la mamafia wa wizi wa mabenki na utekaji. Alifungwa gerezani humu baada ya kumteka mfanyabiashara tajiri wa kutupwa bwana Charles F. Urschek na kujipatia kiasi cha dollars 200,0000.
(II). Alivin Fransis Karps.
Mbabe huyu alikuwa kiongizi wa kundi lililoitwa "barber-Karpis" mbishi huyu pekee ndiye mfungwa aliyekaa miaka mingi katika gereza hili kwa miaka 26.
Alcatraz ilikuwa limegawanywa katika blocks nne, block A, B, C na D, chumba cha Mkuu was Gereza, chumba ya wageni, Maktaba na Saluni ya kunyolea wafungwa, huku block "D" likiwa ndio block hatari zaidi kwa msoto kiasi kwamba pamoja na uhalifu wao katika uhalifu, watukutu hawa waliligwaya sana block hili!.
Gereza lilizungushiwa uzio wa umeme. Hatari zaidi ni kwamba gereza lilijengwa kwenye kisiwa kilichozungukwa na maji ya baridi mno pande zote huku yakiwa na mkondo mkali sana.
Mazingira haya ndio yaliyolifanya gereza hili kuwa la kipekee na kuaminika kuwa gumu kuliko yote kwa mfungwa kutoroka.
Watemi waliopata kupitia ndani ya Alcatraz mara kadhaa walinukuniliwa wakisema
"haikuwa sehemu salama kwa kiumbe chochote kilichoumbwa na Mungu kuishi", kulikuwa na ukatili na maisha magumu sana, watemi walipata shuruba Kali kutoka kwa walinzi lakini wao kwa wao walifanyiana ukatili mkubwa mno. Mfungwa "Edward Wulke" ni mmoja wa watukutu aliyekutana na ukatili humo ndani, huyu alikatwa mikono yake kwa shoka na baadae alikuja kujinyonga.
Mazingira yalikuwa machafu mno kama inavyofahamika magerezani, kazi ngumu kwa muda mrefu huku likiwa ni kawaida sana kupitisha Siku tatu hadi nne bila kula.
Block "D" ndio lilikuwa kiboko yao hii ilikuwa na selo zilizochimbwa shimo, yaani ukiingizwa humu lazima uzame kwenye maji kama usiposimama. Pia humu kulikuwa hakuna umeme na kulikuwa na baridi Kali sana, huku wafungwa wanakuwa nusu uchi. Vitanda kamwe havikuwa vikipatikana ndani ya block D, wafungwa walitembea peku peku, harufu mbaya ilikuwa nyumbani kwake!
Mmoja wa watu waliopata kuishi anakili kwamba Alcatraz ilikuwa ni kama jehanum na kama wangepewa nafasi ya kuchagua kuishi humo na kifo basi wangechagua kifo.
Kiufupi watukutu hawa walikuwa ni kama wafu walio hai, hadi hapo walikuwa na wazo moja tu, kutoroka Au uendelee kuwa maiti inayoishi Alcatraz.
Ndani ya miaka 29 ya uhai wa gereza hili, yalifanyika majaribio zaidi ya 14 yakihusisha watu 46, kati ya hapo wawili walikufa maji, sita walipigwa risasi, 23 walikamatwa na watatu hawajulikani walipo hadi sasa!.
Mtu wa kwanza kujaribu aliitwa Joseph Bowers juhudi zake ziliishia mikononi kwa walinzi, walipigwa risasi baada ya kugoma kutii amri ya kujisalimisha.
Baaadae Theodore Cole na Raph Rae walikuja kufanikiwa kutoroka baada ya kukata nondo ya dirisha lakini wakafia majini kutokana na baridi kali.
June 11 mwaka 1962 wabishi watatu, Frank Morris, John Anglin na Clearance Anglin walifanikiwa kuvunja mwiko wa gereza hili kwa wafungwa kushindwa kutoroka. Hawa walikuwa wakiishi kwenye sello ndani ya block "B" ambako pembeni ya sello yao lilikuwa na korido isiyolindwa, walichofanya ni kutoboa tundu kuunganisha selo yao na korido, shughuli ilifanywa kwa kutumia vijiko na drill walizochomoa kwenye mota ya cleaner, na walifanya kazi hiyo pindi unapopigwa mziki ili kuepuka kusikika wakichimba. Baadae waliondoa feni kwenye roof, na kuweka nondo ambazo ziliacha uwazi wa kupita. Hapa walitumia faida ya korido kutokuwa na walinzi na kuwa sehemu yenye giza, siku ya kutoroka walitengeneza vinyago walivyovivika nywele na kuviweka sehemu wanazolala ili kuwapoteza walinzi.
Baada ya tukio hili FBI walifanya upepelezi kwa muda wa miaka 7 hadi mwaka 1969 walipofunga kesi hii bila kuwa wameona miili ya hawa jamaa wala kujua walipo, wakaamua kuhitimisha kwamba jamaa walikufa maji!.
Hadi sasa kuna utata juu ya hilo, kwani wapo wanaodai watukutu hawa walifanikiwa kutoroka salama na wamekuwa wakiwasiliana na ndugu zao na kwamba walishawahi baadhi yao kuonekana Rio de Janeiro Brazil.
TAFADHARI WAJUZE RAFIKI ZAKO WAIDOWNLOAD APP HII ILI WASIPITWE NA NAKALA ZAIDI TAMU ZA KUSISIMUA

Comments

Popular posts from this blog