REHEMA WA NJIA PANDA(08)
- Get link
- X
- Other Apps
''Una uhakika funguo za mlango ule unazo wewe pekee?" lilikuwa ni swali lililomuumiza yule
daktari kwani licha ya kudai alikiwa nazo peke yake lilikuwa ni uongo ambao yeye na mtu
mmoja ambaye alitamani kutaka kujua kama alienda mahali pale.
Lile swali lilizidi kumuumiza kila dakika licha ya askari polisi kuondoka pale na kuamuahidi
kurudi muda wowote ama kumwita pale watakapomhitaji...endelea
'Kwa nini alirudia sana lile swali atakuwa anajua nini?" yule daktari alijikuta akiongea peke
yake badala ya kufikiri kama alivyotaka kufanya jambo lililomfanya ageuke huku na huko kujua
kama kulikuwa na kiumbe yeyote aliyemsikia.
Hakuwako.
Alishusha pumzi na kupeleka kidole chake shavuni alikopasua kichunusi kilichokuwa kimeiva
na kumsababishia muwasho.
Alikunja uso kwa maumivu matamu ya kutumbua kichunusi kila kabla ya kuchukua kikaratasi
alichojifuta nacho mahali alipotumbua na kupaka damu na majimaji yaliyokuwa yakionesha
kuwa alikuwa amemaliza uhai wa kile kichunusi.
Alisimama ,akakaa alitamani kulalia meza lakini akaona si vyema bali aende tuu nyumbani
kupumzika baada ya kufanya kazi kucha pale hospitalini lakini tena akajikuta akikumbuka tukio
zima la usiku ule hadi mfanyakazi yule wa serikali wa mkoa alipogundulika kutoweka
hospitalini katika mazingira ya ajabu.
Tukio hilo lilimfanya akose maamuzi kwani alijikuta akisimama na kukaa kitini pale ofisini
kama vile palikuwa na mtu aliyekuwa akimwimbisha ule wimbo maarufu shule ya msingi wa
simama kaa..
Hatimaye alipata wazo ambalo aliona lingempa mwanga kidogo juu ya jambo lile.Aliinuka na
kutoka ofisini mwake ambako tangu wale askari polisi watoke aliamua kujifungia.
Kwa mwendo wa haraka aliliacha geti la hospitali na kuelekea nje huku akili yake ikimtuma
kuonana na mtu mmoja ambaye alimpa umuhimu mkubwa kwa wakati ule kwani alijua kabisa
angempa mwanga fulani juu ya jambo lile mtu huyo hakuwa mwingine bali Sikitu msichana wa
kinyamwezi aliyeamua kumweka kama kimada cha muda mrefu.
Kuna kitu ambacho alitaka kukijua kutoka kwake na kitu hicho aliamini kingempa ujasiri wa
kulifikiria na kuliongelea lile jambo kwa uhuru na namna nyingine kabisa.
Akiwa hana hili wala lile njiani huku mwendo wake ukipungua kadiri dakika zilivyosogea
kutokana na fikra alishtuka baada ya kupigwa fimbo ya mgongo iliyomfanya ageuke baada ya
kuachia tusi zito la nguoni ambalo lilikuwa miongoni mwa sifa zake mbaya kwani ilifikia hatua
alikuwa akiwatusi hata wagonjwa waliokuwa wamemuudhi akiwa kazini tabia iliyomweka
kwenye orodha ya madaktari waliokalishwa vikao vingi vya kupewa onyo na kusuluhishwa na
wagonjwa.
''Hahahahah! Ulijifanya umeniweza kunifungia mle ndani leo utalala wewe hahahaha! '' sauti ya
mzaha ilimtoka mtu aliyekuwa amechafuka kwa mavumbi na uchafu wa matapishi uliokuwa
kwenye nguo alizokuwa amevaa kabla ya kumchapa fimbo nyingine ambayo ilimzindua yule
daktari kutoka kwenye kumtafakari mtu ambaye alimwona alikuwa akimtia wazimu kumfikiria
baada ya kutoroka hospitali kimaajabu .
Alitaka kuongea kitu lakini , yule kichaa aliyekuwa mbele yake alimwashiria kugeuka kwa
kidole kuangalia kilichokuwa nyuma yake naye hulka ya udadisi ilimfanya ageuke kuangalia
kulikoni akijipangia kugeuka kwa nusu sekunde na kumchunga yule kichaa aliyemwona kwani
alihisi ni mbinu ya ama kukimbia au kumchapa fimbo nyingine ya mgongo.
''Baba sina tegemeo tena'' aliongea mwanamke aliyekuwa akija mbele yake akilia.
''Nini mama?" aliuliza yule daktari kwa wahka.
''Siki''
''Kafanya nini mama?"
Mama Sikitu badala ya kumjibu aliinua macho kuelekea upande alikokuwa yule kichaa ambaye
siku moja iliyopita aliitwa Anord mfanyakazi wa serikali mkoani akiwa kama afisa manunuzi wa
mkoa wa Tabora, jambo ambalo yule daktari alilifanya lakini alishuhudia Anord akichota vumbi
chini na kuijimwagia kichwani kama vile mtu achotavyo maji yaliyomo kwenye beseni kwa
viganja vyote vya mikono yake na kuoga ama kuosha kichwa.Kila mmoja alijikuta akiahirisha kumtazama Anord na kumwangalia mwenzake na kujikuta
wakigonganisha macho na wote kwa aibu walikwepesha macho yao kwani kabla ya kutembea na
Sikitu yule daktari alikuwa akitembea na mama yake Sikitu jambo ambalo hapo nyuma lilileta
matatizo makubwa kati ya mtu na bintiye.
''Siki amefariki"
"Nini...Amefariki..?!
Itaendelea.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment