REHEMA WA NJIA PANDA(07)

Usiku mzima kelele zilitoka kwenye chumba alimokuwa amelalala Anord na siku iliyofuata
asubuhi ulitawala ukimya kitu kilichowaaminisha kuwa alikuwa amelala usingizi mzito.
Nesi wa zamu akiwa ametanguzana na daktari waliusogelea mlango wa kile chumba ili
wampeleke chumba kingine na kile chumba kitumike kwa ajili ya sindano na oparesheni
ndogo.Walipofungua mlango walipogwa na butwaa kwani walichokishuhudia hawakuwa
wamekitarajia.�....endelea....!!=
Daktari na muuguzi wa zamu hawakuona walichokitegemea zaidi ya kitanda kilichokuwa
kimebinuliwa juu chini.Kwa haraka wakainua kitanda kuona kama palikuwa na mtu pale chini
lakini napo hawakuona chochote zaidi ya mashuka yaliyokuwa yamechafuliwa na matapishi
kuonesha kuwa aliyekuwa amelala juu ya kile kitanda alikuwa ametapika sana kutokana na
uchafu uliokuwa umechafua zile shuka.
Uchunguzi wa kile chumba ulithibitisha kuwa hakukuwa na mtu yeyote zaidi yao.
''Huyu mtu kweli alilala humu ndani?" aliuliza yule daktari akiwa haamini kabisa alichokioba
kwani jana yake alimwacha yule mgonjwa mle ndani baada ya kusumbua wagonjwa wengine
katika wodi.
Yule muuguzi wa zamu hakuwa na jibu lolote kwani hakuwepo wakati yule mgonjwa
akipelekwa kule lakini alipewa tuu maelezo wakati akiingia zamu.Japokuwa alikuwa
akimfahamu Anord lakini hakujua hadi analetwa pale alikuwa na hali gani.
''Si tumekuta mlango umefungwa?" aliuliza yule daktari akiwa bado haamini kilichokuwa
kimetokea.
''Ndiyo huenda akawa ametoroshwa na ndugu zake na kukimbilia kwa waganga wa jadi.
''Kama kutoroshwa basi mlango ungevunjwa mbona mlango upo salama na tumekuta
umefungwa?"
''Huenda waliomtorosha walikuwa na funguo''
''Acha mawazo ya kipumbavu nani ana funguo za huu mlango zaidi yangu?" Alifoka yule daktari
na kuanza kuondoka kwani alijua yule muuguzi alikuwa akianza kumwingiza kwenye uhusika
wa tukio lile kwani ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kutoka mle chumbani na ndiye pekee
aliyekuwa na funguo za mlango wa kile chumba.
Lakini wazo la kusema alikuwa ametoroshwa na ndugu zake lilipuuzwa na ukweli kuwa Anord
hakuwa na ndugu pale Tabora zaidi ya Mbeya hivyo uwezekano wa kutoroshwa na ndugu
ulikuwa mdogo sana.
Taarifa za Anord kutoweka kiajabu chumbani alikokuwa amefungiwa kupunguza kero kwa
wagonjwa wenzake zilienea kama moto wa kiangazi kwenye pori zee na kusababisha
minong'ono miongoni mwa kila aliyelisikia jambo hilo ,kuna walioamini kuwa alitoroshwa kwa
ushirikiano wa mmoja wa wauguzi waliokuwa zamu, kuna waliokuwa wakiamini kuwa Anord
hakuwekwa humo usiku uliopita na kuna wale waliona tukio lile lilihusisha nguvu za kiimani
zaidi huku wakihusisha matukio ya mgonjwa huyo wakati alipokuwa akilalamika kupigwa kofi
wakati alikuwa amejipigiza kitandani.
''Nilikuambia yule kijana ana jini''Alinong'ona mmoja wa wagonjwa akimwambia mwenzake
ambaye alionekana kukubaliana naye kwa kulitafakari jambo hilo na kuuliza swali ambalo
lilikuwa ni kama la kukazia alichokuwa ameambiwa.
''Kwa hiyo anaweza akawa ametoroshwa na hilo jini?"
''Ndiyo , huenda ikawa hivyo maana wanadai mlango ulikutwa kama ulivyokuwa umeachwa''
''Labda ''Hao waliishia kuwaza hilo .
Daktari aliyetoa wazo la kumfungia Anord peke yake na kuondoka na funguo aliona kabisa
jambo lile likimwelemea hasa baada ya askari kadhaa kuanza kuwahoji maswali kadhaa kuhusu
tukio hilo la aina yake lililoharibu kabisa ratiba nzima ya siku ile.
''Una uhakika funguo za mlango ule unazo wewe pekee?" lilikuwa ni swali lililomuumiza yule
daktari kwani licha ya kudai alikiwa nazo peke yake lilikuwa ni uongo ambao yeye na mtu
mmoja ambaye alitamani kutaka kujua kama alienda mahali pale.
Lile swali lilizidi kumuumiza kila dakika licha ya askari polisi kuondoka pale na kuamuahidi
kurudi muda wowote ama kumwita pale watakapomhitaji .�itaendelea,KWA MAONI TEMBELEA PAGE YETU YA FACEBOOK IITWAYO "BONGO TREND".

Comments

Popular posts from this blog