NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU(1&2)
- Get link
- X
- Other Apps
MATESO na shida ni sehemu ya maisha ya mwanadamu lakini kwa upande wangu yalikuwa tofauti na
kujiona naishi dunia nyingine tofauti na wanayoishi wanadamu wenzangu. Kwa hili Mungu atanisamehe
kwa kuamini Mungu aliyekuwa nikielezwa kuwa mwingi wa rehema na huruma kutokana na mafundisho
ya dini yangu hayupo na kuniacha peke yangu.
Niliamini kama angekuwepo niliyokutana nayo yalikuwa na tofauti kubwa na wanadamu wenzangu.
Kucheka kwangu kulikuwa kwa bahati mbaya zaidi ya muda mwingi kuwa nalia huku nikiamini huenda
mimi si kiumbe wa dunia hii kwani hata nyumba za ibada na mafundisho ya dini havikuweza
kuninyamazisha kilio changu hata kunifuta machozi yaliyokosa kizuizi kila kukicha.
Kifo nacho kilinikimbia kila nilivyokikimbilia kama sehemu ya kuepuka tabu za dunia hakikutaka
kuonesha ushirikiano kwangu. Niliwaonea wivu wote niliosikia wamejiua kwa kujinyonga au kunywa
sumu, lakini si kwangu kila hila nilizofanya ili nami nife lakini kifo kilinikataa na kusema hakina urafiki na
mimi.
Nilijiuliza sina raha mateso kila kukicha toka nilipokuwa tumboni kwa mama yangu, suluhu nyepesi
ilikuwa ni kifo nacho kilinikana katukatu hakinihitaji. Hebu niambie ni kiumbe gani kilichokosa yote hayo.
Ni kweli maandiko ya vitabu vitakatifu yalitueleza mwenye dhambi ndiye anayestahiri adhabu, lakini kwa
upande wangu dhambi hiyo niliifanya lini ikiwa mitihani ilianzia toka kutunga kwa mimba yangu.
Vitabu vya dini vinatueleza kuwa mtoto hatahukumiwa kwa dhambi ya mzazi wake, vile vile mzazi
hatahukumiwa kwa makosa ya mwanaye. Kama nivyo basi naamini kabisa japo nipo katika dunia ya
kawaida lakini niliishi dunia ya peke yangu isiyo na Mungu wenye upendo na huruma.
Najua maneno yangu yameutikisa moyo wako na kujiuliza kwa nini niseme maneno yanayoonesha
kabisa namkufuru Mungu na kuamini naishi dunia ya peke yangu. Wakati hakuna dunia nyingine zaidi ya
hii kwani baada ya maisha ya duniani kuna maisha mengine kutokana na imani za dini zetu baada ya kifo
kuna maisha mengine ya milele peponi kama umetenda mema au motoni (jehanamu) kama umetenda
mabaya.
Nakuomba unipe muda wako ili ujue nimekutana na mambo gani yaliyonifanya nikufuru Mungu na
kuamini hayupo. Naitwa Mwanani jina maarufu ambalo nimekuwa nalo japo jina la kusomea shule
niliandikishwa jina la Salha. Elimu yangu kidato cha pili, si kwamba sikuwa napenda kuendelea
na masomo, yote haya yalianza miaka miwili baada ya kifo cha mama yangu mpenzi.
Kwa kweli kila ninapohadithia mkasa huu moyo wangu huwa unakufa ganzi kwani maisha yangu yalianza
misukosuko toka nikiwa tumboni baada ya ujauzito wangu kutaka kutoka baada ya kipigo cha mbwa
mwizi alichokipata mama toka kwa baba baada ya kumshtumu alikuwa akitembea na mfanyakazi wa
ndani na ujauzito wangu si wake.
Unaweza kujiuliza yote haya nimeyajua wapi wakati mama yangu kufariki nikiwa na miaka kumi sita na
wakati huo nilikuwa nimeanza darasa kidato cha kwanza. Mengi nilielezwa na bibi baada ya kuona
nategwa na mtu niliyefahamu kuwa ni baba yangu mzazi. Pia kunieleza maneno mazito ambayo nilipata;ufafanuzi mpana toka kwa bibi kizaa mama kijijini.
Malalamiko yangu niliyapeleka kwa bibi kutengwa na baba pia kuelezwa kuwa mimi si mtoto wake eti
nina baba yangu wakati mama yangu alipokuwa hai hakuwahi kutamka. Wakati huo kidogo akili ilianza
kufanya kazi wakati huo nilikuwa na umri wa miaka kumi na sita.
Baada ya kumueleza bibi manyanyaso niliyokuwa nayapata kutoka kwa baba yangu. Bibi alinieleza kisa
kimoja ambacho kwa kweli kilinitisha na kunifanya nianze kupoteza mwelekeo wa maisha kwa kuamini
sikuwa na haki toka kwa baba niliyemtegemea.
“Mjukuu wangu napenda kukueleza jambo moja ambalo halikuwa siri tulilijua hata sisi wa pembeni
lilikuwa wazi kwa kila mtu alilijua. Mama yako kweli alikuwa mwingi wa habari nilimuonya mara nyingi
ikawa nafanya kazi bure sawa na kutwanga maji kwenye kinu hakuwa muaminifu katika ndoa yake.
“Baba yako alikuja kunishtakia mara nyingi kuwa mama yako si muaminifu, nilimwita na kumueleza
malalamiko ya mumewe, lakini yaliingilia kushoto na kutokea kulia. Mara ya mwisho aliwafumania
wakifanya mapenzi na huyo mfanyakazi wa ndani.
“Mjukuu wangu napenda kukueleza jambo moja ambalo halikuwa siri tulilijua hata sisi wa pembeni
lilikuwa wazi kwa kila mtu.
“Mama yako kweli alikuwa mwingi wa habari, nilimuonya mara nyingi ikawa kazi bure sawa na kutwanga
maji kwenye kinu, hakuwa muaminifu katika ndoa yake.
“Baba yako alikuja kunishtakia mara nyingi kuwa mama yako si muaminifu, nilimwita na kumueleza
malalamiko ya mumewe, lakini yaliingilia kushoto na kutokea kulia.
“Mara ya mwisho aliwafumania wakifanya mapenzi na huyo mfanyakazi wao wa ndani.
“Kutokana na baba yako kumpenda sana mkewe, alimfukuza mfanyakazi lakini aliendelea na mama
yako, kwa bahati mbaya mwaka huo huo ndiyo mimba yako ilipoingia.
“Japo kitanda hakizai haramu lakini baba yako aliikataa mimba yako kwa kuamini mwenye ujauzito huo
ni yule kijana.
“Kutokana na maelezo ya baba yako kabla ya ujauzito wako, miezi karibia miwili mama yako alikuwa
akimnyima unyumba baba yako kwa kisingizio cha kuumwa.
“Kumbe usiku alikuwa akimtoroka mumewe kitandani na kwenda kufanya mapenzi na mfanyakazi,
kijana dhalili ambaye hakuwa na mbele wala nyuma.
“Mjukuu wangu nilisema mpaka mdomo wangu ukataka kupasuka lakini sikio la kufa siku zote halisikii
dawa.
“Basi tangu ujauzito wako ulipotungwa palizuka mifarakano mikubwa huku baba yako akilazimisha
mimba yako itolewe. Lakini mama yako aligoma na kumueleza hata kama hatamhudumia basi
angekuhudumia yeye.Siku moja waligombana sana huku baba yako akimpiga mama yako tumboni ili kuhakikisha kwamba
mimba yako inatoka.
“akini Mungu mkubwa pamoja na kuumizwa sana, bado ujauzito wako haukutoka. Muda ulipofika,
mama yako alijifungua salama mtoto wa kike ambaye ni wewe.
“Hata hilo jina la Mwanani maana yake ni mtoto wa nani kwa vile ulikataliwa na baba yako. Baada ya
kuzaliwa sura yako ilifanana sana na yule mfanyakazi hapo ndipo palipozuka chuki huku ukitafutiwa kila
njia ya kukuliwa bila mafanikio.
“Mara ya kwanza mama yako alikuja huku alikaa mpaka baba yako alipokubali kukutambua kama
mwanaye na kukubali kukupa huduma zote kama mtoto wake hata kadi yako ya kliniki alikubali
liandikwe jina la kaka wa baba yako mzazi.
“Kwa vile mama yako alijua baba yako hana mapenzi na wewe ya kweli alikununulia kiwanja ili
akujengee nyumba kama urithi wako akiwa hai kwa kuamini akifa mapema hutapata kitu kwa baba yako.
“Lakini kwa bahati mbaya mama yako alifariki kabla hajatimiza dhamira yake, kwa kweli mpaka leo sijui
mwanangu aliugua ugonjwa gani. Toka niishi katika dunia hii na umri wangu sijawahi kuuona ugonjwa
huo.
“ Mama yako alipoingia katika siku zake za mzunguko wa hedhi alitokwa na damu mfululizo ambazo
hazikukoma mpaka alipokata kauli.
“Kwa kweli baba yako alikuwa akimpenda sana mama yako, alipoteza fedha nyingi kuokoa maisha yake
lakini hakufanikiwa. Hata kifo cha mama yako kilimliza sana. Kama utakumbuka alikonda sana baada ya
kifo mama yako.
“Baada ya kifo chake kulizuka tetesi kuwa ule ulikuwa uchawi aliofanyiwa na mwanamke mmoja
aliyekuwa akitembea na mume wake. Kwa hilo siwezi kumkingia kifua kwani mama yako kwa kweli
alikuwa mwingi wa habari. Nina imani ulimuona, Mungu alimjalia sura na umbile zuri basi, alifanya
chochote alichokitaka bila kuogopa aibu.”
ITAENDELEA........
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment