JE WAJUA...?!


By@bin cypher™
Mnamo Mwaka 2006, wiki kadhaa baada ya kustaafu nafasi ya ukatibu mkuu, Kofi Annan alienda nchini Italia kwa ajili ya mapumziko.
Akiwa huko, Siku moja aliamua kutoka nje kidogo na kwenda kununua gazeti, lakini ghafla akashangaa Watu wengi wanamzonga. Lengo lao ni kutaka sahihi kutoka kwake. (Kama uonavyo nyota wa filamu au wachezaji mpira, wanavyochora sahihi zao kwenye mashati ya wafuasi).
Lakini kumbe, Watu hao walimfananisha Kofi Annan na yule nyota wa filamu wa marekani bwana Morgan Freeman .
Ila, kwa kutotaka kuwaangusha Watu hao, Kofi Annan alichora sahihi kwa kutumia jina la Freeman.
(Angalia picha zao)
Koffi Anan, alifaliki akiwa na umri wa miaka 80 huko nchini Switzerland.
Alihudumu nafasi ya ukatibu mkuu kwanzia Mwaka 1997 hadi 2006, akiwa ndiye mwafrika mweusi wa kwanza kushika nafasi hiyo.
RIP koffi Annan.

Comments

Popular posts from this blog