REHEMA WA NJIA PANDA(06)

Dakika arobaini zilipokuwa zikisha ndipo wote walikuwa wakishuka mlima mrefu ambao
walikuwa wameupanda tena wakiwa wakikimbia mtu wa kwanza kushtuka alikuwa Sikujua
ambaye ni kama alikuwa akirejewa na fahamu na kujishika siri yake ambayo haikutamanika
kwa kulowanishwa na dafu lililokuwa nimepasuliwa na kumwagiwa maeneo hayo�....Endelea.....
''Paah!'' kibao kilichotua kwenye shavu la kushoto la Anord na kumzindua kutoka kwenye
umbumbumbu uliotokana na shughuli aliyotoka kuifanya.
''Mbona unanipiga Siku kulikoni?" Alilalama Anord akijipapasa shavu lake lililokuwa
limepigwa.
''Umefanya nini mpumbavu wewe?"
''Nimefanya nini ama tumefanya nini?" Aliuliza Anord akicheka.
''Mpumbavu mkubwa wewe umeona nakuchekesha hapa'' Hapo kofi la uso lilitua usoni
likifunika jicho lote na kuumsababishia Anord atoe ukelele wa maumivu.
''Mamaaaa nakufa!"Sauti ilimtoka Anord na kuwashtua wagonjwa na Kisebengo ambaye alikuwa
ameanza kusinzia kutokana na ukimya wa mgonjwa wake.
''Nini tena Anord?" Aliuliza kwa wahka Kisebengo huku akijutia kitendo cha kujiingiza kwenye
matatizo ya Anord ambaye alijua kabisa kuwa palikuwa na kitu kilichokuwa kikiendesha suala
lile.
''Nimepigwa kofi la uso ''
''Na nani wewe umepigwa wapi?"
''Jicho la kushoto halafu limevimba'' Alijieleza Anord wakati huo wagonjwa kadhaa walikuwa
karibu na kitanda cha Anord wakishangaa maneno aliyokuwa akiongea kwani kuna waliokuwa
wakimshuhudia anavyojipiga kwenye pembe ya kitanda cha chuma alichokuwa amelalia.
''Mzee si umejigonga kitandani mara mbili, mara ya kwanza shavuni na mara ya pili kwenye
jicho lako la kushoto sasa hilo kofi la kukutoa nundu umepigwa saa ngapi?" Aliuliza kijana
mmoja aliyekuwa amelala pembeni yake akimwangalia Anord tangu alivyoanza kuhangaika
kujigeuza huku na kule saa nyingine akilamba hewa na shuka lake.
''Kweli ona hata nywele zimebakia hapa" aliongea mgonjwa mwingine ambaye alikuwa kwenye
kiti cha matairi.
'' Anaweza akawa na jini huyu si bure'' Alichangia mada mmoja aliyekuwa kwenye kundi la
wagonjwa wagonjwa waliokuwa wamesimama kukizunguka kitanda cha Anord.
''Hapana huenda ni maralia imepanda kichwani''aliongeza mwingine.
Baadaye alikuja daktari kumpa dawa za maralia kama vipimo vilivyoonesha awali huku
akishtushwa na uvimbe uliokuwa jichoni ambao ulionekana kuongezeka kadri muda ulivyozidi
kupita .Baadaye Anord alijikuta usingizini lakini tofauti na mara nyingine usingizi ule ulimtisha
na kuanza kupiga kelele ambazo zilimwamsha mwenyewe huku akionekana kama mgonjwa wa
akili lakini kwa vipimo vya daktari vilionesha kuwa alikuwa na maralia kali ambayo kama
walivyodai ilikuwa imekimbilia kichwani.
Hali ilikuwa hivyo kila alipopata usingizi na baada alianza kukimbia na kama si madaktari na
wagonjwa wachache waliokuwa na nguvu basi Anord angepotelea mitaani huko huku akipiga
kelele zilizokosa maana yoyote kwa kila aliyezisikia.
Madaktari walichukua uamzi wa kumfunga kamba lakini kila alipopata usingizi alijikuta akipiga
kelele huku akitaka kukimbia jambo lililokuwa kero kwa wangonjwa wengine hatimaye
akahamishwa chumba na kupelekwa kwenye chumba cha upasuaji mdogo na sindano
kulikokuwa na kitanda kimoja ili afungiwe huko hadi asubuhi kwani muda huo ilikuwa saa mbili
na nusu usiku.
Usiku mzima kelele zilitoka kwenye chumba alimokuwa amelalala Anord na siku iliyofuata
asubuhi ulitawala ukimya kitu kilichowaaminisha kuwa alikuwa amelala usingizi mzito.
Nesi wa zamu akiwa ametanguzana na daktari waliusogelea mlango wa kile chumba ili
wampeleke chumba kingine na kile chumba kitumike kwa ajili ya sindano na oparesheni
ndogo.Walipofungua mlango walipogwa na butwaa kwani walichokishuhudia hawakuwa
wamekitarajia
ENDELEA KUSAMBAZA HADITHI HII ILI IWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI,ASANTE

Comments

Popular posts from this blog